SOMA KISA HIKI AFU SHAURI.
Here is what's in store for your love life.
kuna Kijana amenicheck akiomba ushauri, ana Mke ana miaka 24 na yeye ana miaka 28 , story yake iko hivi, Ana Mwanamke amemuoa na hawajabahatika kupata mtoto,anasema alipofunga nae ndoa, Mwanamke huyu alikuwa mjamzito, na aliamini ule ujauzito ni wa kwake, na ata alipomua alisisitiza sana nisimtelekeze, na alisema kiumbe aliekuwepo tumboni kwake ni wa kwangu , sasa sababu nilikuwa na vijisenti nikapambana nikatoa mahari nikiamini kiumbo ni wangu haraka sana nikamuoa , Tukalea mimba miezi nane ilivyofika mara siku hio damudamu na maji vikatoka kumbe Mfuko wa uzazi ulipasuka hivyo tulienda hospitali na alifanyiwa upasuaji huku kiumbe kikiwa kimetolewa kikiwa hai , haikuwa ridhiki mtoto yule aliishi siku 13 na baada ya hapo alifariki huku akituachia majonzi lakini maisha yalivyo tuliendelea kuishi na kusahau kabisa maumivu, kuna siku Diva nikaja kujua mke wangu ana wasiliana na mtu jinsia ya kiume wakifokeana na kutukanana kama walishindwana vile, nikaja kujua walikuwa wanawasiliana kwa njia za message nimesoma wakijadili kiumbe huku mke wangu akisema wewe si ulinitelekeza mtoto alizaliwa na alikufa, wakati nasoma zile message nilishtuka sana , kumbe sikuwa baba wa yule mtoto yule ambae nilihangaika sana kwa kila kitu hadi Mungu anamchukua, sikupenda sana kuendelea sababu ni kiumbe cha Mungu na hakuwa na kosa, napata sana changamoto ya mawazo, ukizingatia hakuna hata mtu mmoja niliemwambia haya mambo, niko nayo kifuani hata mke wangu hajui, nawaza nimueleze ukweli juu ya alichokifanya au nimuandikie talaka ,kwasasa nimempa likizo fupi akatulie kwa wazazi wake kidogo sababu mimi nilipata safari kikazi nikawa nae mbali kidogo, kwao sio mbali sama nikirudi nitamfuata hamna shida, naomba ushauri nimpe talaka hukohuko aliko au nifanyaje?


cha msingi ni kuendelea na maisha hakuna mkamilifu wapo wenye matatizo makubwa zaid ya hayo keep it up lets go
JibuFuta