CCM yatangaza ratiba ya vikao vya kitaifa jijini Dodoma kuanzia Agosti 21, 2025
Vikao hivyo, vinavyoongozwa na Mwenyekiti wa CCM Taifa, Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, vitahusisha Kamati Kuu (CC) na Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC). Ajenda kuu: ✅ Uteuzi wa wagombea Ubunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ✅ Wagombea wa Viti Maalum ✅ Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar ✅ Wajumbe wa Viti Maalum vya Baraza la Wawakilishi Vikao hivi vinatazamwa kama hatua muhimu kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Oktoba mwaka huu, vikitarajiwa kuvuta hisia kubwa kutoka kwa wanachama na wananchi kwa ujumla. #DivaMediaAfrica #CCM #Dodoma #Uchaguzi2025









