HAKUNA MBADALA WAKE
Mwimbaji maarufu kutoka Nigeria, Davido, ameonyesha wazi mapenzi yake ya dhati kwa mke wake Chioma akisema kuwa yeye ni sehemu ya maisha yake ambapo hakuna mtu mwingine anayeweza kuchukua nafasi yake.
Davido alifunguka katika mahojiano, akieleza historia yao ya muda mrefu tangu wakiwa shuleni. Alisema mara ya kwanza alipoanza kumjua Chioma alimvutia kwa uelewa, utulivu na hekima, akibainisha kwamba daima alikuwa ni mtu anayejua kuzungumza naye moja kwa moja badala ya kusambaza maneno kwa wengine.
Mbali na hilo, Davido alimuelezea Chioma kama binti mwenye heshima kubwa, anayejua kupika aina zote za vyakula na mwenye moyo wa upendo. Alisimulia kumbukumbu ya siku ya kwanza Chioma alipokuja nyumbani kwake na kuandaa chakula, akimuita mlinzi na mfanyakazi wa ndani kushiriki chakula pamoja na familia. Tukio hilo lilimfanya Davido kuthibitisha kuwa Chioma ana sifa zote za kuwa mke bora.
Kauli hiyo imekuja kabla ya sherehe yao ya White Wedding iliyofanyika Miami, ambapo wawili hao walionekana wakithibitisha tena mapenzi yao hadharani.



Maoni
Chapisha Maoni