ZUCHU MPYA NA AMANDA
Msanii wa Bongo Fleva Zuchu ametoa tamko zito kwa mashabiki wake akieleza kuwa anaingia kwenye awamu mpya ya muziki wake. Kupitia InstaStory, ameandika:
“This is the new me. I will be as versatile as I want to be… kama unahisi mabadiliko haya huyawezi, tu ni bora uniachie sasa… Maana huko naelekea hutovielewa kabisa.”
Zuchu amesema hataki kukaa kwenye comfort zone tena, na sasa ataendelea kuchallenge sound yake kila siku. Amesema mabadiliko haya si kwa kila mtu, na anaelewa kuwa sio mashabiki wote watamuelewa lakini kwa wanaomsapoti, “funga mkanda maana safari ndio kwanza inaanza.
Mashabiki wamemjia juu, wengine wakimkumbusha ngoma kama Idibala na Prakatatumba zilivyokuwa “zisizo na maana”
lakini zilipendwa.
Zuchu anasema:
East Africa tumejaliwa wasanii wakali na yeye yuko tayari kuleta tuzo za Grammy.
Je, uko tayari kwa Zuchu mpya?
Habari kamili inapatikana kwenye App ya Diva Media Africa



Maoni
Chapisha Maoni