SIMBA WATUA SALAMA SUDAN
Klabu ya Simba SC imewasili salama nchini Sudan kwaajili ya mechi za kirafiki Tatu zitakazo pigwa nchini humo
Klabu hiyo itakuwa na mchezo mitatu ya kimataifa na klabu Za Asante Kotoko, ambayo itakuwa mechi ya awali kabisa itakayochezwa siku ya Tarehe 28 Agosti mwaka huu.
Ikifuatiwa na mechi ya pili dhidi ya AL Hilal mnamo tarehe 31 ya mwezi huu huu pia itamalizana na timu ya As Arta Solar.
Ikumbukwe Timu ya Arta Solar imecheza mchezo wa kirafiki na timu ya KMC katika dimba la Uhuru siku ya Tarehe 25 na matokeo yakiwa ni sare pacha ya 1-1 huku klabu hiyo ikiwa na Nyota wa zamani kutoka Barcelona Alex Song huku pia kiungo wa zamani wa simba Thadeo Lwanga alicheza katika mchezo huo.
Katika michezo hiyo mitatu Kocha Zaran pia amethibitisha kumuwekea sawa mchezaji Victor Akpan ambaye awali alisema hayupo katika mipango yake, Kocha huyo pia aliweka orodha ya wachezaji kadhaa amabo hawatokuwa katika mipango yake ikiwemo mchezaji Kapama Nasoro ambaye alisajiliwa kabla ya Kocha huyo Kuingia klabuni hapo .
Michezo hiyo ni kwaajili ya kujiweka sawa kwaajili ya michezo ya kimataifa ya Ligi ya mabingwa Barani Afrika Ambako simba wanaanza na klabu ya Big Bullets mwezi Septemba.






Maoni
Chapisha Maoni