Umalaya Tena Basi - 2 Face

 


2Face Idibia(2Baba) akiri kutokuwa mume bora pia kutokuwa baba bora kwa watoto wake na kuomba radhi kwa mke wake, watoto wake, wanawake aliozaa nao na kuomba radhi familia za pande zote , 

Amesema hataki huruma wala kujaribu kujifanya mtu mzuri wala hatafuti kiki ila anamaanisha anachosema kwani ameona mweyewe amekuwa akiwasababishia aibu mke wake, watoto wake, mama yake mzazi, familia za pande zote na wanawake wengine aliozaa nao, Amesema ameamua kubadilika na kuahidi pia kuwapa muziki mzuri mashabiki wake

2Face ambaye ana miaka 46 ana watoto 7 aliozaa na wanawake watatu tofauti wakiwemo wawili aliozaa na mke wake wa sasa Annie Idibia(37). Pia amemshukuru mkewe kwa kuendelea kuwa nae pamoja na kusema ni mwanamke wa aina yake

Ikumbukwe msanii huyo mara kadhaa amekuwa akikumbwa na skendo ikiwemo za wanawake na mambo ya familia kuwa hadharani pia 

Hata hivyo,  inadaiwa pia sababu mojawapo ya kujiitokeza kuomba radhi ni kwamba tayari ameisaliti tena ndoa yake kwa kuchepuka na mdada anayefanya kazi benki na kumpa mimba

Maoni

Machapisho Maarufu