NILIUMIA SANA BAADA YA KUACHANA NAE - SHAKIRA
Mkongwe na Superstar mkubwa duniani Shakira Aliyeiteka Dunia Miaka ya nyuma na kubadilisha ladha ya tasnia ya muziki kwa style zake za kucheza zenye asili ya kiarabu kitendo kilichomfanya azidi kujinyakulia umaarufu na kupata mashabiki wengi uku akitangaza muziki wa latino duniani kote...kama mnakumbuka mwaka 2010 alipata nafasi ya kuandika wimbo maalumu kwa ajili ya kombe la dunia lililofanyika barani afrika na kutumbuiza wimbo huo pia ndoto ya kumpata ampendae ikakamilika baada ya kukutana na mchezaji wa spanish aitwae Gerard Pique na kuanzisha mahusiano ambayo yalidumu kwa muda mrefu.Mwaka 2013 alimwambia ELLE kuwa "Alianza kufikiria uwenda Hakuna Mungu, ghafla nikakutana na Gerard na jua likachomoza.
Muda umebadilika,, japokuwa anaandaa kuachia albamu yake ya kwanza mpya baada ya miaka 5 kupita, kwenye exclusive interview na ELLE kutoka nyumbani kwake Barcelona 'Ameelezea jambo hili analiona kama ni MASAA YA GIZA... mwezi wa sita alitangaza kuachana kwake na gerard na ugumu uliopo juu ya kupata haki ya kulea wanae (milan 9, Sasha 7) bado serikali ya spain inamshutumu kukwepa ulipaji wa kodi tuhuma ambazo alizikataa , tarehe kamili ya hukumu haijatajwa bado.
nyota ya shakira ilianza kung'aa tangu akiwa msichana eneo la barranquilla, colombia akijishughulisha na michongo ya uchimbaji wa madini, alipofikisha umri wa miaka 14 alisikia kuna mkurugenzi anafanya usaili wa kusaka vipaji vya waimbaji ndipo alipoanza kujifunza lugha ya kingereza na kwenda nchini marekani. Akapata Umaarufu mwaka 2001 alipoachia albamu u iitwayo "Laundry service"
Akaanza kujihusisha na kazi za kijamii pamoja na siasa na kutengeneza shule maeneo ya alipozaliwa "Muziki umesababisha yote haya" umekuwa kishawishi kikubwa kwangu.
Alifanya mazungumzo kwa mara ya kwanza na ELLE na kuweka wazi kuhusu albamu yake mpya, anguko la mahusiano yake na tamanio la kuzungumza kuhusu uchumi wake. Nimekuona ukisheherekhea siku ya kuzaliwa ya baba yako mzazi? Ukamzawadia wimbo "ulikuwa ni mzuri"..ndio ni shujaa wangu ni mfano wa hekima , amekuwa rafiki kwangu, mshauri bora napohitaji ushauri lakini kwa bahati mbaya alikuwa na mwaka mgumu alikuja barcona baada tu ya kusikia matatizo ya familia yangu na alikuja kunipa sapoti lakini ugonjwa wa ubongo ulimuangusha vibaya na kumpelekea kufanyiwa upasuaji wa ubongo na wiki moja baadae akaanguka tena na kuvunja mifupa mingi usoni mwake.
Mungu wangu! Kwahiyo imekuwa mwaka mgumu kwake lakini ni ushuhuda wa nguvu yake na bado anacheza akisikia mziki mzuri uku akijaribu kuimba, nimetambua pia zawadi bora ya kuwapa wazee wetu sio uwepo wetu tu bali mziki ukifikiria nguvu ya mziki inanifanya nitambue kuwa kazi yangu sio yakuwa shujaa kama daktari au nesi au mwanajeshi vitani lakini kwa namna moja au nyingine mziki unanjia ya kuunganisha watu na maisha.
Sitaki kukuuliza kuhusu muziki wako kwasababu una albamu inakusubiri na haujatoa albamu tangu mwaka 2017..ndio! Nina albamu nzima imebeba thamani kubwa ya mziki inayonifanya niwe mwenye furaha kwani nyimbo zingine mtazisikia nikiwa nimeshirikiana na wasani, zingine nimeimba kwa lugha ya kingereza na kihispania zenye ladha tofauti lakini ninafuraha sio sababu ya kile nilichokianda kwa ajili ya wale watu wanaosubiri bali yale niliyoyafanya wakati naanda albamu hii. Nilidhani nimemaliza albamu yangu lakini kila nilipoingia studio kukamilisha wimbo fulani au kuchanganya ladha ya wimbo fulani naishia kuandika wimbo mpya kwasababu najihisi kuwa mbunifu zaidi'.
Nambie kidogo kuna mahusiano gani kati ya muziki wako na unayoyapitia kwa sasa" nadhani kila mmoja ana njia yake ya kukabiliana na huzuni, hofu au msongo wa mawazo" wote tunapitia magumu kwenye maisha lakini kwa upande wangu nadhani kuandika muziki inanisaidia kupata majibu ya maswali yangu napokuwa na huzuni pia upendo kutoka kwa familia yangu na wanangu unanisaidia kuona wepesi wa mambo "" nadhani muziki ni kama tegemeo langu" kuna nyakati zingine inanibidi kujipambania niwe sawa na njia pekee ya kufanya hivyo ni kupitia muziki,,,unajua kujipa nafasi ya kujitathamini inanifanya nitambue kuwa mimi.








Hellow my
JibuFuta