Mke Wangu anaishi Oman - Kivurande

 


Morning Guys .

leo Taifa La Tanzania linalia majenereta Tu huko Nje , anyways nahisi i need to Update this , Jana Nilipata Bahati Ya Kuwa na Kivurande katika show yangu ya lavidavi wasafi saa 4 usiku mpaka saa 6 na tuliongea sana kuhusu muziki wake na Maisha Yake kwa Ujumla, vingi vilihusu hasa Muziki wake wa Kibao Kata , Gladly alikuja na Mke wake anaishi Oman,

Tuliogusia Ni usaliti na alidai amekuwa katika wakati mgumu kama Supastaa sababu watu wana M DM sana mke wake na kumwambia habari za uongo kuhusu yeye ila ndani ya miaka yao 6 ya ndoa hajaawahi tetereshwa na habari hizo, na amekiri huwa wanaonana mara 6 kwa mwaka hivyo huzuia hisia zake na kulinda uaminifu wake na halali wala kujihusisha na mwanamke mwengine sababu Penzi lake liko kwa Mke wake lakini aliongezea kuwa wanaume ni wa Chepukaji sana na wanawake wengi wamekuwa wakilizwa na wanaume sababu sio waaminifu na kati Ya Vitu aligusia sababu Muziki wake una mashabiki wengi wa kike ni ile hali ya kusumbuliwa kimapenzi na wanawake wakiamini yeye ni fundi wa Mapenzi , nikamuuliza wewe ni fundi kweli? akasema sana Yeye Ni Fundi na anapenda sana Mapenzi sababu hanywi Pombe havuti sigara wala bangi,

Msanii Huyu Ni Mbondei wa Muheza Tanga.

Angalia apa 



Maoni

Machapisho Maarufu