Good Morning , leo nimeamka na mjadala huu apa ,Nilitamani nifanye Podcast bt MIC yangu imeharibika so ntaandika na kuandika na kuandika ata kikijaa kitabu ntaandika and maybe ni bora ata nipate na kitabu aisee ndoto yangu ya miaka na miaka na miaka ..
Mjadala wa Leo Huu. Ndoa Ndoano kwa kila Mwanandoa.
Kwann ndoa inageuka kuwa vita?
Kwann unashauri watu vizur tu na wanafanikiwa why wewe mwenyewe yanakushinda .. truthful hakuna yanayomshinda mtu .. Sisi wote binadamu , hakuna aliekamilika .. unaona yanamshinda mtu sababu anakuelezea .. akikaa kimya akajifanya yuko happy unaweza hisi ana matatizo yake ? so ni watu waongee au wakae kimya maana dunia imeharibika huwezi amini mtu tena katika maisha yako. hao tunaita marafiki ndio hawafai unaongea nae anaenda kuyamwaga sasa only way is to keep it to yourself au tafuta Therapist ongea nae tena awe Professional. nje ya nchi wapo na wamejaa kibao hela yako tu elimu siku hizi mpaka online unapata.
Sasa ngoja niongee ...
Atakushauri nini wakati ndoa yake mwenyewe imemshinda? Comment ya Kipumbavu kabisa kwa watu wapumbavu.
Anaeshindwa na ndoa ni nani? Mwanamke Mtulivu au Mwanaume Malaya ?!
Tuanze na Mwanamke mtulivu ... Viuno waganga Tabia Njema havimtulizi mwanaume kwenye ndoa , Kama Hulka Yake Malezi Yake Na Makuzi Yake ni tatizo basi huyo mtu ni tatizo (mental health issues Pia ni tatizo sana ) Kama Circle yako ni negative energy umbea na unafiki my dear brother ndoa yako Pia itakuwa hivyohivyo ndio maana sio kila mtu unamkaribisha ndani kwako na kuleta mazoea kwa mke wako au kuwapa chance ata ya kutoa maoni kuhusu mke wako inshort wewe mwenyewe ndio utatengeneza heshima au kuacha avunjiwe heshima, waliosoma cuba mmeelewa.
Hawa Mawifi ndoa zao zinawashinda na kufundwa kwao na kupewa kitchen Party yake inamshinda au imemshinda ndio utegemee aje kukutengenezea yako na mkeo , kama una dada fyatu muweke mbali na mkeo, tena mbali hasa na uwe mkali kama una dada muelewa na mwenye upendo keep the sister hood. kuna wadada kazi yao kuuza kaka zao kwa wanawake wengine kwa maslahi yao binafsi , vihela vidogodogo njaa ni kitu kibaya sana aisee ... kujidharaulisha na kujichoresha kwa kupenda vya bure same applies kwa mashemeji na wasio jielewa.
In laws aisee hasa wamama baadhi yao ni kipengele sana even in the movies tunaona wanaitwa monsters in law na sio Mother in law , ukipata alie na upendo na umama akakupenda na kukulea kama mwanae shukuru Mungu sana most of them wanataka wakutumie kwa faida zao vitu ambavyo watoto wao wameshindwa kuwafanyia na ukigoma kugeuzwa atm my dear hufai wewe utapigwa vita vya wazi na vya mambo meusi kama hujaaga kwenu ndio boom byebye ila kama umeaga kwenu na Mungu Yu Pamoja nawe ni vile Mungu atakulinda vitapita angani. hawana jema no matter what you do ndio mana utaona watoto wao hawakai ktk ndoa awe wa kike au wa kiume.
Jengine nalo ni laana za familia .. hili tunahitaji watu wa kiroho sana waje watufungukie na tena wakemee pia hii ni tatizo sana.
wanawake wengi wametulia sana katika ndoa zao wanaofanya ushenzi ni wanaume sasa hao ndio ndoa zimewashinda , kila ndoa ina changamoto zake karibia 99.9% matatizo ya ndoa yanafanana ni vile kuna waliowazi ku share na kuna wanaoficha ili wasionekane wadhaifu kushare ufuska wa Partner wako sio udhaifu ni ushujaa,
Na kosa ni wewe unaejua huyu ana mke unatembea nae na yule anaejua nina mke na anakitembeza ovyo kosa si la yule aliendani ni la wewe unaetoka nje, kuna kitabu nimesoma na nta share na nyie apa .. Kwann mwanaume anakukana hadharani ... Jibu rahisi sana hakupendi!. hakuna sijui namtumia mtu kwa ajil ya umaarufu wala hela hapana simply ushatumika shughul imeisha anakukana sababu hakupendi na hataki kuumiza anaempenda sababu yako , wanasema wanaume wameumbwa kwa udhaifu lakini je unajisikiaje? kakutumia kakuvua nguo kakumwaga, hajali machozi yako uliolia kisa kampost mkewe wala hajibu message zako na kakublock kisa hataki ndoa yake iharibike , unahisi kwenda kwa waganga kumvuta na kumlipua au kumuharibia maisha kutakusaidia nini ? hapana unapoteza muda wako .. umeachwa kubali move on hakupendi amekutumia kwa maslahi yake binafsi na hayuko proud hajawahi kuwa proud na wewe ndio maana pia alikuwa anakufichaficha na kukudanganya daily.
There’s nothing in life quite as wonderful—and challenging—as marriage. We strongly encourage all couples to be proactive in identifying and seeking help for speed bumps before they turn into full road blocks. Schedule a yearly marriage "check-in" to keep your relationship heading in the right direction as you walk together in your journey through life ...
kuishinda ndoa inabidi uwe na imani na Mungu Sana , Maana Kuna Usaliti Uongo Ukandamizaji na kuna wanaokuzunguka waliojaa unafiki uliokithiri huku na huku wapo wakuitwa mawifi na mashemeji na marafiki 85.5% tabia zao zinafanana (snitching) yan hili ni tatizo huku wapo kule wapo afu kupe balaa.
Hakuna Mwanamke ndani anaeanza kuwa jeuri na kufanya vitu tofauti kama wewe Mwanaume haukuwa chanzo ya mabadiliko ya Mwanamke huyo Shetani umemtengeneza wewe na usione mtu yuko kimya na anafanya vitu vyake ni amejitafuta amejipata.
Wanasema Divorce is not the only option but sometimes Divorce is a Peace of Mind kujiepusha na mental health au vifo visivyotarajiwa tumeona watu wakimaliza a kisa ndoa siku hizi kila wakati hali hii hu reportiwa na vyombo vya habari, wanawake usaliti wao unatokana na nini? na wewe Mwenyewe hulka za Kimalaya au tabia za kutengenezeka zinazoletwa na wale wanaopenda kushauri ndio maana tunashauriwa kusikiliza zaidi au kueka block ktk nani wa kukushauri , sababu huyo anaekushauri nae ana yake pia ambayo hawez kukueleza so akili za kuvukia barabara muhimu sana. huongo husambaa zaid kuliko ukweli na chunguza sana sio kila unachoambiwa kinaukweli lakini Pia usishangae kuona wanandoa waliogombana leo kesho wamepatana Hio ndio Ndoa Ndoa Ndoano!.
Ndoa zinavunjika Pia siku Hizi sababu Ya Kipato, Generational curses , Social Media , Circle Ya ajabu (Marafiki na ndugu)
Lack of commitment, financial challenges, and infidelity, lack of sympathy trust and respect.
Ndoa Ni nini ?! Ni Ya Watu Wawili.
the legally or formally recognized union of two people as partners in a personal relationship (historically and in some jurisdictions specifically a union between a man and a woman). "a happy marriage.
Kiafrica ndoa ni kila mtu kutia mdomo wake , ukosefu wa nidhamu kama mtu hajawahi tia neno ktk ndoa yako kwann wewe unatia neno kwenye ndoa ya mwenzio au unahisi huyo Mume wako ni mwema katulia? you should know better , why ubomoe ya Mwenzio wakati yako unaipalilia. Ndoa sio ile sherehe na makaratasi mliopewa ndoa ni ile sasa mnaanza kuishi knowing Mema na Mabaya aisee ni kivumbi leo!.
ntae
Kwanini ndoa huanguka ?! Kuna uvumilivu kuisha lakini hasa Mapenzi kuisha and are you happy? mabaya mangap mazuri mangap? ushawahi fanyia ndoa yako kazi ? Michepuko nao ni topic tofauti, akiwa na Mume wa mtu atatafuta njia yule
mke ajue .. tena kwa waislamu ndio akiambiwa ataolewa mke wa pili anajitoa ufahamu au wa tatu au wanne mwisho wa siku mke akijua ni utaachwa au kufedheheshwa.
kwann michepuko inapenda drama ?! kwann wakidhalilika mtu huyo hutengenezewa zengwe? is it a sin kurudi kwa mke wake au alikuaminisha nini hasa ukahisi atakuwa na wewe milele , who told you Moyo hupenda wawili? moyo una space moja tu kwa mtu umpendaye no matter what he wil always go back to her. lakin why kila wakat na wewe unampokea anaekupiga matukio yasio na heshima? stil mjadala kuhusu ndoa ni endless.
kumbuka wanaotaka utoke ktk ndoa yako wanataka uwe miserable. Je unaweza irekebisha? imekushinda? then give it to God. ask him to do it for you my dear waganga watakula tu hela zako God is the only way. kama ni wako atabaki kwako kama si wako utapita na utapata alie wako. hakuna njia tofauti Mahi dear. kuna ndugu ambao wamefeli maisha miaka 30 imemkuta hana mbele hana nyuma hawa wako tayar kukuharibia muonekane mko sawa.
Kuna mtu aliwahi niambia Mama Yangu ananifatafata sana katika ndoa yangu sijui alitaka au anataka nimuoe yeye kila mtu nikiwa nae hamtaki ni kamwambia usiseme hivyo badala yake kaa nae mwambie kila usichopenda kuhusu yeye ili ajue na ajue mipaka yake jaman baba mkwe nae yan Mume upate baba mkwe anaempenda binti yake utaisoma namba utajuta na Mama mkwe anaempenda Mwanae wa kike ndio wewe mwanaume utisoma namba pia , ila kuna mama mkwe wa Mume anataka uoe familia nzima na kuwahudumia watahamia kwako na wakufundishe jinsi ya kuishi na binti yao ni utasomesha familia na kuhudumia mpaka utajiuliza nimeoa familia nzima au kwahio hii issue aisee ni panaaa mnoooo, kuna wanaume wanajuta kuoa vikao kila saa na baba mkwe binti yangu kasema hivi na vile jamani kidogo binti kwao utaitwa utasemwa weeeee na umdondokee kwa kulipa hela kwa ufupi jamani ndoa hizi ukiskiza matatizo yao utasema bora langu maana wengine hufuma waume zao kitandani na dada wa kazi marafiki na sasa mmoja alimfuma mumewe na mwanaume mwenzie mbona shughuli ushetaniiii umejaa yarab . kubambikiziwa je watoto? kama Hujui DNA utalea sana watoto sio wako, wanawake wanatembea na ma house boy ma bodaboda na mashemeji kwahio ukiwasikiliza wanaume ya kwao utachoka. kuna mwanaume juzi kawe kagundua mkewe anatoka na boda na jirani na rafiki ake kipenzi na watoto wale wote sio wake, alitamani kunywa sumu. jaman trust me jipende sana wewe mwenyewe kwanza at the end of the day self love will never hurt you. put you first shobo za ndoa Punguza.

Part 2 inakuja na ntaomba ushirikiano wenu ktk kuiandika ..
whatsapp me 0754479898 niongezeeni fikra zenu.
Maoni
Chapisha Maoni