NASHINDWA KULALA KITANDANI KWANGU

 


Hi guys , theres a lot to blog today.

leo nimepata nafasi ya kuangalia interview ya niite bosheni, nimejisikia huzuni sana , sababu situation ya mwanae ni situation ambayo nimekulia, nilifichwa mazingira ya kifo cha mama yangu mpaka nakuwa naona akili inafanya kazi ndio nikagundua mamangu alifariki nilipo mdogo na mama angu mkubwa hakuwa mamangu bali alinilea na alikuwa ananiambia mimi sio mama yako na nililelewa na bibi na babu yan ilikuwa ukitaja mama tu unaambiwa wewe nyamaza, kiukweli sio sahihi uwazi na ukweli ni bora kwa afya ya akili, nahisi namuelewa sana huyu kaka anasema anashindwa hata kulala nyumbani kwake  kitanda walichoshare hawezi lalia  , walipeana ahadi yeye na haitham kwangu MIMI NI MWANAMKE WA MAISHA YAKO NA WEWE NI MWANAUME WA MAISHA YANGU hio kauli inamuumiza sana , anasema familia ya Mke wake inakataza  mtoto asione picha za mamake na asijua kama mamake amefariki anasema hio hali hakubaliani nayo sababu atakuwa na atagundua alifichwa mazingira ya kifo cha mamake, anataka mwanae ajue mamake alifariki alipokuwa mdogo na yeye kama babake ndio amebeba jukumu la kumlea na kumsaidia, anasema uwezo wa kumlea mtoto wake anao, anasema hajawahi zoea kifo cha haitham mpaka Leo.


Maoni

Machapisho Maarufu