NILITOBOLEWA KOO ASEMA PROF J

 

'Rapa' Mkongwe na Mbunge wa zamani wa Mikumi, Joseph Haule (Prof. Jay) amesema Ugonjwa wa Figo ulimuweka Chumba cha Uangalizi Maalum (ICU) kwa siku 127 huku safari ya kuumwa kwake ikichukua takriban siku 462 ambapo alifikia hatua ya kutobolewa Koo ili kuondoa uchafu uliosababisha ashindwe kuongea


Akizungumza zaidi, Msanii Black Rhyno ambaye ni mdogo wa Prof. Jay amesema kuna wakati kaka yake alipata hali ya Moyo kusimama mara 3 katika vipindi tofauti lakini juhudi za Madaktari na huruma ya Mungu zilimnusuru na kifo mkongwe huyo


Aidha, Prof. Jay akizungumza na Clouds FM amesema Ugonjwa huo ulimlazimu kuchoma Sindano 10 zilizogharimu Tsh. Milioni 50 na baadaye alipelekwa Hospitali iliyopo India, na hilo limemsukuma kuanzisha 'Foundation' itakayohusika na masuala ya kusaidia Wagonjwa wa Figo.

amemalizia angependa kuonana na Mama Samia Amshukuru 

Maoni

Machapisho Maarufu