SHAKIRA KIKAANGONI
Hi Guys wusap!
anyways mmeona story ya shakira ?! Nilikuwa Jamii forums nacheck zangu news nkakutana nayo!.
Nyota wa Muziki wa Pop na Raia wa #Colombia, #Shakira amefikia makubaliano na Waendesha Mashtaka wa kumaliza Shauri la kukwepa Kodi kwa kulipa Euro Milioni 7.5 (Tsh. Bilioni 20.4) kabla kesi ya msingi haijaanza kisikilizwa
Awali, Shakira alitakiwa achague kulipa kiwango hicho ili mambo yaishe au Shauri liende Mahakamani na akishindwa kesi kuna kifungo cha Miaka 8 jela na Faini ya Euro 23.8m (Tsh. Bilioni 65), akachagua Mahakamani kabla ya kubadili mawazo baadaye
Shauri la Msingi lilikuwa kukwepa Kodi ya Euro Milioni 14.5 (Tsh. Bilioni 39.4) lililowasilishwa Mahakama ya Barcelona



Maoni
Chapisha Maoni