Zuchu Ampiku Yemi Alade
Nyie ZUCHU hashikiki.
Zuchu amefanya mambo makubwa katika tasnia ya muziki, na ni jambo la kushangaza kuona anafikia mafanikio mapya kwenye YouTube.
kwa ufupi Amefikisha wafuasi milioni 3.01 kwenye YouTube, na kuwa msanii mwanamke aliye na wafuasi wengi zaidi katika eneo la Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara.
Amemzidi Yemi Alade wa Nigeria, ambaye alikuwa msanii wa kwanza mwanamke wa Kiafrika Kusini mwa Jangwa la Sahara kufikisha wafuasi milioni 2.
Ni jambo la kujivunia sana kwa Zuchu na nchi yake!



Maoni
Chapisha Maoni